Storm FM

Ujenzi daraja la Magufuli wafikia 76%

11 September 2023, 10:08 pm

Mwonekano wa daraja la Magufuli Kigongo Busisi. Picha na Mrisho Sadick

Serikali imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Magufuli la Busisi-Kigongo jijini Mwanza ambalo linatarajiwa kukamilika mapema mwaka kesho.

Na Mrisho Sadick – Geita

Ujenzi wa daraja la Magufuli la Kigongo Busisi jijini Mwanza umefikia asilimia 76 huku likitarajiwa kukamilika mwaka kesho na kuanza kutoa huduma kwa wananchi na gharama ya ujenzi huo ni zaidi ya shilingi bilioni 700.

Hayo yamebainishwa  na msimamizi wa mradi huo Mhandisi William Sanga wakati Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Geita ilipotembelea ujenzi wa daraja hilo lenye urefu wa kilomita 3 na barabara unganishi zenye kilometa 1.66 huku katibu wa CCM mkoa wa Geita Alexandrina Katabi akipongeza hatua hiyo.

Sauti ya msimamizi wa mradi na Katibu wa CCM
Halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Geita ikikagua daraja la Kigongo Busisi. Picha na Mrisho Sadick

Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Nicholous Kasendamila wamemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa kuendelea kutoa fedha za utekelezaji wa mradi huo.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Geita na Mwenyekiti wa CCM

Kukamilika kwa daraja hilo kutapunguza muda wa kuvuka hadi dakika 5 kwa kutumia gari na dakika 15 kwa watembea kwa miguu kulinganisha na muda wa wastani wa dakika 25 hadi 45 kwa kutumia kivuko, nakuwa kichocheo kikubwa cha uchumi.