Storm FM

DED, RMO, DC Geita waongoza mazoezi ya viungo

18 May 2024, 2:21 pm

Kutoka kushoto ni DED, DC na RMO Geita wakiongoza mazoezi ya viungo. Picha na Juma Zacharia

Wilaya ya Geita imeendelea na ufanyaji mazoezi ya viungo vya mwili tangu utaratibu huo ulivyoanzishwa na DC Hashim Komba yakiwakutanisha watu mbalimbali.

Na: Juma Zacharia – Geita

Mazoezi hayo yaliyopewa jina la “Geita Fitness Time” yameanzia Nyankumbu senta hadi uwanja wa CCM Kalangalala yakijumuisha viongozi mbalimbali akiwemo mkuu wa wilaya ya Geita, mkurugenzi wa mji wa Geita Yefred Myenzi, wafanyakazi wa halmashauri, taasisi mbalimbali, wananchi pamoja na wanafunzi wa shule tofauti tofauti wilayani Geita.

Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Geita Yefred Myenzi amesema kuwa mazoezi ya viungo yana faida katika ujenzi wa Taifa kwa kuwa nguvu kazi iliyo na afya inatimiza majukumu yake sawa sawa.

Sauti ya DED Mji wa Geita
Wananchi mbalimbali waliojitokeza kufanya mazoezi ya viungo. Picha na Juma Zacharia

Mwanzilishi wa zoezi hili mkuu wa wilaya ya Geita hashimu Komba akizungumza baada ya mazoezi hayo amesema kuwa mwezi ujao Mkuu wa mkoa wa Geita Martin Shigela atakuwa mgeni katika mazoezi hayo.

Sauti ya DC Geita

Naye mganga mkuu wa mkoa wa geita Omary kisukari amesema kuna baadhi ya magonjwa ambayo yanaweza kuepukika kwa kufanya mazoezi

Sauti ya RMO Geita

Ikumbukwe kuwa mazoezi haya yamefanyika leo kwa mara ya pili baada ya mwezi uliopita na sasa yatafanyika tena mwezi juni.