Storm FM

Mwenge wa Uhuru wafika kwa Hayati JPM

7 August 2023, 10:33 pm

Picha na Mrisho Sadick

Mpaka sasa, mwenge umezunguka katika wilaya tano na halmashauri sita ndani ya mkoa wa Geita, ambapo umepitia miradi 59 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 29 na kutembea umbali wa kilometa 770.

Na Mrisho Sadick- Geita

Mwenge wa Uhuru ukiwa wilayani Chato mkoani Geita umefika nyumbani kwa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli  na kutoa heshima kisha kuendelea na shughuli zake.

Picha na Mrisho Sadick

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka huu Abdallah Shaib amewaongoza wakimbiza mwenge na viongozi  mbalimbali kuingia nakutoa heshima kwa Hayati magufuli.

Mwenge huo ukiwa Wilayani Chato umekagua na kuweka mawe ya msingi katika miradi 7 yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 13.

Picha na Mrisho Sadick

Mbunge wa Jimbo la Chato Mhandisi Medard Kalemani pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Chato Deusdedith Katwale wamemshukuru Kiongozi wa Mbio za Mwenge huku wakimuomba kufikisha salamu za pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kupeleka miradi  na fedha ndani ya Wilaya hiyo.