Storm FM

Kinana azindua ofisi za kisasa za CCM Bukombe

13 December 2023, 4:00 pm

Makamu mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abrahman Kinana (wapili kushoto) akizindua majengo ya ofisi za CCM Bukombe. Picha na Zubeda Handrish

Wilaya ya Bukombe imetekeleza Ilani ya chama cha mapinduzi CCM kwa kujenga ofisi za kisasa.

Na Zubeda Handrish- Geita

Makamu mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abrahman Kinana, amezindua ofisi ya kisasa ya chama hicho wilayani Bukombe mkoani Geita ambapo ofisi hiyo imejengwa sambamba na mgahawa, jengo la mapumziko pamoja na ukumbi wa mikutano.

Sauti ya Makamu mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abrahman Kinana, Sauti ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Bukombe Dkt. Dotto Biteko na Mkuu wa mkoa wa Geita Mh. Martine Shigera.

Kinana amewapongeza viongozi na wanachama wa CCM kwa ushirikiano wao katika kujenga chama hicho huku skiongeza kuwa ni moja ya utekelezaji wa Ilani ya CCM sura ya 10, Ibara ya 246 inayoeleza mambo yanayotakiwa kufanyika ndani ya miaka 5

WanaCCM katika uzinduzi wa ofisi Bukombe. Picha na Zubeda Handrish

Kwa upande wake Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Bukombe Dkt. Dotto Biteko amemshukuru Makamu Mwenyekiti TZ bara Kinana kwa kufika na kuzindua majengo hayo.

Nae Mkuu wa mkoa wa Geita Mh. Martine Shigera amezungumzia baadhi ya miradi ya maendeleo mkoani Geita na katika wilaya ya Bukombe iliyokamilika na inayoendelea kutekelezwa.