Storm FM

Umoja wa wanawake wilaya ya Geita Kumuenzi JPM kwa kuchapa kazi

5 April 2021, 1:23 pm

Jumuiya ya umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi wilaya ya Geita umesema wanawake watamuenzi Hayati  Dkt John Pombe Magufuli kwa kuchapa  kazi na kusimamia haki na kumuunga mkono Rais wa awamu ya sita  Samia Suluhu Hassan ili kutimiza maono ya mtangulizi wake.

Tamko hilo limetolewa na Bi Antonia Charles Lubadila mwenyekiti wa UWT  Wilaya ya Geita wakati wa uzinduzi wa kituo cha ushonaji na utengenezaji nguo za batiki kinacho milikiwa  na kikundi cha wanawake  kata ya katoro mkoani Geita.

Stephania Benjamini na Maimuna Mingisi Madiwani wa viti maalumu katika wilaya ya Geita wamezungumzia kifo cha Hayati  Dkt John Pombe Magufuli alivyowabeba akinamama wakati wa uongozi wake na kuwasaidia kukuza uchumi wao na walivyoridhika na uteuzi wa Rais  Samia Suluhu Hassan na Makamu wake Dkt Philip Mpango.