Storm FM

Jamii Yaaswa Kuwaelewa Wajawazito

8 June 2021, 3:37 pm

Na Zubeda Handrish:

Jamii imetakiwa kuwa na uelewa juu ya  hali anayopitia mwanamke katika kipindi cha ujauzito ambacho mara nyingi hupelekea mwanamke kuchagua baadhi ya vyakula pamoja na hasira.

Hayo yamezungumzwa na Daktari Victor Kajoba kutoka hospitali binafsi ya SAKAMU iliyopo mjini Geita na kusema kuwa hali hiyo inatokea kutokana na mabadiliko ya vichocheo vilivyopo katika mwili wa mwanamke na sio kwamba wanawake hufanya mksudi kama inavyotafsiriwa na baadhi ya wanajamii.

Katika hatua nyingine Dokta Kajoba amewashauri akina baba na wanafamilia kuzingatia taratibu za rishe bora kwa akina mama wajawazito ili kuepuka changamoto za kiafya kwa mama na mtoto ikiwemo baadhi ya akinamama mujifungu watoto wenye uzito pungufu.

Aidha baadhi ya wananchi wamesema  hali hiyo inapotokea kwenye familia zao waelewe kuwa ni jambo la mpito na kuacha tabia za kuwanyanyapaa baadhi ya akin mama wajwazito kutokana na hali hiyo.