Storm FM

Watu 25 wakamatwa tuhuma za madawa ya kulevya

5 August 2023, 8:12 pm

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib aliyekatikati akizungumza na wakazi wa wilaya ya Geita. Picha na Mrisho Sadick

Serikali imeendelea kujenga mizizi katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa kuuanda klabu za kupinga matumizi hayo katika shule za msingi na sekondari.

Na Mrisho Sadick:

Watuhumiwa 25 wa dawa za kulevya wamekamatwa na kufikishwa mahakamani wilayani Geita ikiwa ni mwendelezo wa mapambano ya kuzuia  biashara na matumizi ya dawa za kulevya hapa nchini.

Akisoma taarifa kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwenyekiti wa klabu ya kupinga matumizi ya dawa za kulevya katika Shule ya Sekondari Nyanza wilayani Geita amesema katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Juni 2023 watuhumiwa 25 wa dawa za kulevya walikamatwa , kesi 23 zilifunguliwa na  kesi sita zimehukumiwa huku zingine zikiendelea katika hatua mbalimbali.

Sauti ya Mwenyekiti wa klabu

Katika kipindi Cha Januari hadi Juni Mwaka 2022  madawa ya kulevya aina ya Bangi yaliyokamatwa na watuhumiwa kufunguliwa kesi ni kilo 33.8 za bangi  , misokoto 412 ,kete 85 huku waathirika wakubwa wa dawa hizo wakitajwa kuwa ni vijana.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2023 Abdalla Shaib Kaim amewataka wananchi na viongozi  kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa kutoa taarifa za wauzaji na watumiaji ili kukomesha vitendo hivyo.

Sauti ya Abdala Shaib