Storm FM

Madereva waonywa kupakia dizeli, petroli kwenye usafiri wa umma

18 October 2023, 6:30 pm

Changamoto ya baadhi ya wasafirishaji kuruhusu kupakia chupa zenye mafuta ya dizeli na petroli kwenye vyombo vyaio imekuwa kero kwa abiria mkoani Geita.

Na Zubeda Handrish- Geita

Baadhi ya abiria wanaotumia magari madogo ya abiria aina ya hiace yanayofanya safari zake kutoka Geita mjini- Katoro hadi Chato wamewalalamikia wahudumu wa magari hayo kupakia mafuta ya dizel na petrol katika madumu hali ambayo ni hatari kwa usalama wa maisha.

Abiria hao wametoa malalamiko hayo wakati wakizungumza nakuziomba mamlaka zinazohusika kuchukua hatua za haraka kabla ya madhara kutokea.

Sauti ya abiria wa Geita mjini Katoro
Sauti ya abiria wa Geita mjini Katoro- Chato

Kwa upande wao waendesha vyombo vya moto na wahamasishaji wa magari ya Geita mjini- Katoro hadi Chato wamekiri kuwepo kwa vyombo vinavyopakia madumu ya mafuta kinyume cha taratibu.

Sauti ya waendesha vyombo vya moto na wahamasishaji wa magari ya Geita mjini- Katoro hadi Chato

Kaimu Afisa Mfawidhi wa LATRA mkoani Geita Kenan Katendasa amesema mara kadhaa wamechukua hatua kwa watoa huduma wa usafirishaji wanaovunja sheria za usalama barabarani.

Sauti ya Kaimu Afisa Mfawidhi wa LATRA mkoani Geita Kenan Katendasa
Sauti ya Kaimu Afisa Mfawidhi wa LATRA mkoani Geita Kenan Katendasa