Storm FM

Biteko awataka viongozi kuongeza weledi fedha za miradi

25 September 2023, 10:53 am

Naibu Waziri Mkuu, Waziri wa Nishati na Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Dkt. Dotto Biteko. Picha na Zubeda Handrish

Baada ya kuzindua maonesho ya 6 ya kimataifa ya teknolojia ya madini katika viwanja vya EPZA mjini Geita Septemba 23, 2023, Waziri Biteko alifika hadi kwa wananchi wa Bukombe, mamlaka ya mji mdogo Ushirombo nyumbani kwao kwa ajili ya shukrani.

Na Zubeda Handrish- Geita

Naibu Waziri Mkuu, Waziri wa Nishati na Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Dk. Dotto Biteko (CCM) amewataka viongozi wa kuteuliwa na kuchaguliwa kuongeza weledi katika usimamizi wa fedha za miradi ya maendeleo.

Waziri Biteko ametoa maelekezo hayo jana Septemba 24, 2023 wakati akizungumuza katika mkutano wa shukrani kwa wananchi wa Bukombe uliofanyika katika mamlaka ya mji mdogo Ushirombo wilayani Bukombe mkoani Geita.

Viongozi mbalimbali na wananchi wa Bukombe katika mkutano wa shukrani wa Waziri Biteko. Picha na Zubeda Handrish

Amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anatoa fedha nyingi za miradi lengo ni kuona watanzania hasa wa daraja la chini wananufaika na nchi yao hivo