Storm FM

Wananchi Sungusira waomba zahanati ianze kazi

1 July 2024, 10:32 am

Mwonekano wa nje wa jengo la zahanati ya kijiji cha Sungusira. Picha na Evance Mlyakado

Ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Sungusira kata ya Nzera halmashauri ya wilaya ya Geita unatarajiwa kuondoa adha ya kutembea umbali mrefu kwa wananchi wa eneo hilo kufuata huduma za afya katika vijiji jirani.

Na:Evance Mlyakado -Geita

Wananchi wa kijiji cha Sungusira kata ya Nzera wilayani Geita wameonesha kufurahishwa na hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho huku wakiiomba serikali kukamilisha maeneo machache yaliyosalia ili waweze kunufaika na uwepo wa huduma za afya jirani na makazi yao.

Wananchi hao wamesema kuwa ujenzi wa zahanati hiyo utawaepusha na adha ya kutembea umbali mrefu wa kufuata huduma za afya katika vijiji jirani ikiwemo kijiji cha Fulwe na Nzera ilipo hospitali ya wilaya.

Sauti ya wananchi

Mwenyekiti wa kitongoji cha Sungusira Barnaba John na Mwenyekiti wa CCM kata ya Nzera Nyasuka Nyamhanga wameungana na wananchi kuelezea manufaa ya kukamilika kwa zahanati hiyo huku wakielezea jitihada na hatua zilizofikiwa kwa sasa.

Sauti ya mwenyekiti wa kitongoji
Sauti ya mwenyekiti CCM kata

Kwa upande wake mganga mkuu wa wilaya ya Geita Dkt. Modest B. Lwakahemula na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita Bw. Karia Rajabu Magaro wamesema Zahanati hiyo itafunguliwa mapema mwezi Julai mara baada ya kukamilika kwa miundombinu yote iliyosalia.

Sauti ya DMO na RMO