Storm FM

Wafugaji watakiwa kunenepesha mifugo

31 August 2023, 10:21 pm

Ng’ombe wakiwa na afya duni. Picha na Kale Chongela

Kulisha ng’ombe kwa kutumia aina yoyote ya malisho, haitoshi kuwa na ng’ombe mwenye afya nzuri na maziwa ya kutosha, hili limemuinua Afisa Mifugo na kutoa elimu kwa wafugaji.

Na Kale Chongela- Geita

Wafugaji wa ng’ombe mjini Geita wametakiwa kuipatia mifugo mashudu ambavyo ni vyakula vinavyowezesha mifuguo hiyo kunenepa na kuongeza thamani ya mfugo pindi wanapofikishwa sokoni.

Akizungumza na Storm FM Afisa Mifugo wa halmashauri ya mji wa Geita Bw. Amos Edward Makeja, amesema mashudu ni mojawapo ya vyakula ambavyo vinawezesha mfugo kunenepa na kuongeza  wingi wa maziwa.

Sauti ya Afisa Mifugo wa halmashauri ya mji wa Geita Bw. Amos Edward Makeja

Meneja wa kiwanda cha kuchakata alizeti kilichopo mtaa wa Shilabela Bi. Scola Charles Jige amesema ili kuepukana na changamoto ya uhaba wa mashudu hayo ni vyema wafugaji kununua na kuweka akiba kwa siku za mbeleni.

Sauti ya Meneja wa kiwanda cha kuchakata alizeti, mtaa wa Shilabela Bi. Scola Charles Jige