Storm FM

Mwitikio kuchangia damu Geita mjini ni mdogo

24 July 2023, 1:19 pm

Shabiki wa Yanga Anna Charles akiwa na Mratibu wa damu salama Shabani Makoye akichangia damu. Picha na Kale Chongela.

Uhitaji wa damu salama katika Hospitali ya Halmashauri ya mji wa Geita Mkoani Geita ni Mkubwa kuliko inayopatikana kutoka kwa watu wanaochangia.

Na Kale Chongela:

Mwitikio wa wananchi kuchangia damu salama  bado ni Mdogo ukilinganisha na uhitaji katika Hospitali ya halmashuri ya mji wa Geita.

Kauli hiyo imetolewa na Msimamizi wa kitengo cha damu salama katika Hosptali hiyo Shabani  Makoye  katika zoezi la uchangiaji wa damu lililofanywa na mashabiki wa Yanga katika Mtaa wa Mgogo B kata ya Buhalahala Mjini Geita.

Sauti ya Mratibu wa damu Shabani Makoye

Baadhi ya wananchi waliyoshiriki katika zoezi hilo la uchangiaji wa damu wametumia fursa hiyo kuwataka wananchi na  jamii kuendelea kwakuwa uhitaji ni mkubwa.

Mwenyekiti wa tawi la Yanga Mtaa wa Magogo “B” Robert Sungura  amesema amewahamasisha wananchama wake juu ya umuhimu wa kuchangia damu ili kuokoa vifo vya watu wenye uhitaji wa damu.

Sauti ya Mwenyekiti tawi la Yanga Magogo
Mwenyekiti wa tawi la Yanga Magogo “B”Robert Sungura akichangia damu. Picha na Kale Chongela.