Storm FM
Storm FM
1 June 2026, 5:35 pm

Tukio la kufukiwa wachimbaji hao limetokea May 28, 2026 majira ya saa Alasiri ambapo Jeshi la zimamoto na uokoaji wilaya ya Bukombe limeendelea na zoezi la uokoaji kwa kushirikiana na wachimbaji wadogo.
Na: Edga Rwenduru
Familia za wachimbaji watatu wa madini waliofukiwa na kifusi cha udongo katika machimbo ya mgodi uliopo kijiji cha Kelezia kata ya Igulwa Wilayani Bukombe mkoani Geita wameiomba serikali na wadau kuongeza kasi ya zoezi la uokoaji wa ndugu zao ambao wako ndani kwa siku tano sasa.
Wakizungumza katika eneo la tukio ndugu hao wamesema ipo haja ya serikali kuongeza kasi na nguvu ya kuwaokoa ndugu zao huku wakieleza hofu kwamba muda unavyozidi kwenda matumaini ya kuwatoa wakiwa hai yanazidi kupungua.
Tangu ajali hiyo iliyotokea Mei 28, 2026 majira ya saa tisa alasiri, ndugu hao wameweka kambi eneo la tukio huku wakishuhudia wachimbaji wadogo na Jeshi la zimamoto na uokoaji wakiendelea na zoezi la uokoaji.
Walioangukiwa na kifusi wanatambulika kwa Majina ya Juma Hussein 27 mkazi wa Mtaa wa Shinyanga A,Leonard Charles miaka 29 mkazi wa Masumbwe na Ave Mchele miaka 37 mkazi wa Kalole wote kutoka wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.
Kwa mujibu wa Meneja wa Mgodi huo Peter Joseph Vijana hao waliangukiwa na kifusi cha udongo wakati wakifanya ukarabati ndani ya moja ya shimo linalosadikika kuwa na urefu wa zaidai ya futi 80.
Sikiliza taarifa zaidi na mwandishi wetu Edga Rwenduru.