Storm FM

Nyang’hwale kutoa chanjo ya kichaa cha Mbwa

10 May 2026, 4:58 pm

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye kikao cha Baraza la madiwani Nyang’hwale. Picha na Mrisho Sadick

Chanjo hiyo inatarajiwa kutolewa ndani ya mwezi Mei, 2026, ambapo zaidi yam bwa 2,000 wanatarajiwa kuchanjwa katika kata zote 15 zilizopo ndani ya halmashauri ya wilaya hiyo.

Na Mrisho Sadick:

Halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita imepokea jumla ya dozi 2240 za chanjo ya kudhibiti kichaa cha mbwa zinazotarajiwa kutolewa kwa wafugaji wa mbwa wilayani humo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale, Husna Toni ametoa taarifa hiyo mara baada ya kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo.

Mkurugenzi mtendaji wa Nyang’hwale Husna Toni kushoto akiwa na katibu tawala wa wilaya hiyo Kaunga Amani. Picha na Mrisho Sadick

Amesema hatua hiyo inakuja ikiwa ni mwendelezo wa kudhibiti homa ya kichaa cha mbwa ambayo ni miongoni mwa magonjwa hatari yanayoweza kuhatarisha usalama wa binadamu.

Sauti ya Mkurugenzi
Madiwani wakiwa kwenye kikao cha baraza la madiwani Halmashauri ya Nyang’hwale. Picha na Mrisho Sadick

Diwani wa Kata ya Izunya, Mashaka Jeki,Diwani wa Kata ya Mwingiro Emmanuel Charles na Diwani wa Viti Maalum Hellena Shija wamesifu mpango wa utoaji wa chanjo hiyo kwani ni moja ya mahitaji makubwa katika jamii ya wafugaji kwa ajili ya usalama wao na mifugo yao.

Sauti ya Madiwani