Storm FM
Storm FM
17 April 2026, 1:56 am

“Kila Jambo hapa duniani kwa sasa linategemea elimu, hata mimi leo nisingekuwa diwani kama nisingeweka bidii kwenye masomo ili kutimiza ndoto zangu” – Mgeni rasmi Reuben Sagayika
Na: Ester Mabula
Mahafali ya nne ya kidato cha sita yamefanyika Aprili 16, 2026 katika shule ya sekondari Shantamine iliyopo kata ya Mtakuja, manispaa ya Geita ambapo wahitimu wamehimizwa kujiandaa vyema ili kufanya vizuri kwenye mtihani wa kuhitimu.
Awali wakisoma Risala mbele ya mgeni rasmi, Mkuu wa shule msaidizi Mwalimu Petro Nchalangi na Muhitimu wa kidato cha sita Slama Njau wamesema shule hiyo imepiga hatua kitaaluma katika maandalizi ya mitihani ya ndani na nje huku wakieleza changamoto za kitaaluma na kimiundombinu zinazoikabili shule hiyo.

Mgeni rasmi, Diwani wa kata ya Kalangalala Reuben Sagayika kwa niaba ya mstahiki Meya Leonard Bugomola, ameeleza mikakati ambayo itafanyika ili kutatua changamoto hizo.

Akizungumza Diwani wa kata ya Mtakuja Costantine Morandi amewapongeza walimu kwa kuendelea kuwajenga wanafunzi kimaadili na kitaaluma jambo linalochochea ufaulu mzuri.
