Storm FM
Storm FM
17 June 2026, 6:08 pm

TAKUKURU mkoa wa Geita imeendelea kufatilia na kuchulua hatua juu ya makosa mbambali ya Rushwa kwa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa mbalimbali wa makosa hayo.,
Na: Ester Mabula
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Said Lipunjanje kwa niaba ya Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Geita imeeleza kuwa watumishi watatu wa Manispaa ya Geita walikusanya mapato kupitia mfumo unaotumia mashine za kukusanyia Mapato ya Serikali POS nakwamba watumishi hao wameisababisha Serikali hasara ya jumla ya shilingi 48,067,500 kwa kutokuwasilisha makusanyo hayo kwenye akaunti ya Serikali kinyume na utaratibu.
Watumishi walioshitakiwa na ubadhirifu huo Ally Hassan Semfukwe – Afisa Umwagiliaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita, Edward Cloward Kamugisha – Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita na
Happyness Regness Mushi – Mkusanyaji Mapato wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita.
Katika hatua nyingine TAKUKURU Mkoa wa Geita imewafikisha mahakamani watumishi wanne wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Geita kwa tuhuma ya ubadhirifu wa shilingi 41,987,607.5 uliofanyika katika Akaunti ya Mirathi ya Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Geita.
Watumishi hao waliwalipa wanufaika wawili wasio na madai yoyote ya mirathi Mahakamani, kwa lengo la kurudisha fedha hizo kwa watumishi hao, kupitia miamala ya kibenki na mitandao ya simu, kinyume na utaratibu.
Watumishi walioshtakiwa na ubadhirifu huo ni Bulemo Yuda Mswaga – Afisa Hesabu Mkuu,Mercy Geoffrey Magezi – Msaidizi wa Hesabu,Baldo Donatus Kafene – Mhasibu na William John Mbwambo-Dereva ambao walishirikiana na watumishi wawili Idara zingine za serikali ambao ni Mernad Menard Mbena fundi sanifu kutoka chuo cha utafiti wa madawa Mwanza na David Thomas Moshi muuguzi kutoka hospitali ya Rufaa Bugando.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa kufuatia matukio hayo uchunguzi ulifanyika na baada ya kupata vibali kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashitaka (NPS), watuhumiwa tajwa wamefikishwa Mahakamani Juni ,2026 na kufunguliwa mashauri manne katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Geita.