Storm FM
Storm FM
24 April 2026, 4:25 pm

“Naamini ukarabati wa barabara hizo utaondoa usumbufu kwa wananchi wa kata ya Kalangalala na kuwasaidia kufanya shughuli za kiuchumi” – Diwani Reuben Sagayika
Na: Ester Mabula
Kata ya Kalangalala imeingia mkataba wenye thamani ya shilingi milioni 15 na kampuni ya ukandarasi ya JODECO kupitia fedha zilizotengwa halmashauri ya na Manispaa kupitia mapato ya ndani ili kukarabati barabara zenye urefu wa kilomita 10.3 ambazo ni korofi.
Akizungumza leo Aprili 24, 2026 mara baada ya kutia saini mkataba wa ujenzi wa barabara hizo, Diwani wa kata ya Kalangalala Reuben Sagayika, kila mtaa uliopo katika kata yake utatengenezewa barabara moja korofi.

Mkurugenzi wa Kampuni ya JODECO, Gwasa Balankena, ameahidi kutekeleza kazi hiyo kwa wakati na kwa kuzingatia makubaliano yaliyowekwa huku mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mbugani katika kata hiyo akieleza namna ukarabati huo utakavyosaidia wananchi katika kufanya shughuli zao.