Storm FM

Geita DC na mkakati wa kuongeza uzalishaji mpunga

2 September 2023, 2:13 pm

Mashamba ya mpunga katika kijiji cha Salagulwa wilayani Geita. Picha na Mrisho Sadick

Kutokana na mabadiliko ya tabianchi wakulima wilayani Geita wameishauri serikali kuboresha kilimo cha umwagiliaji ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa chakula.

Na Mrisho Sadick:

Kuboreshwa kwa miundombinu ya kilimo katika halmashauri ya wilaya ya Geita itasaidia kuongeza uzalishaji wa zao la mpunga kutoka tani elfu 63 kwa mwaka hadi kufikia tani laki moja na elfu 40 kwa mwaka.

Hayo yamebanishwa na Afisa Kilimo wa halmashauri hiyo Mariki Athumani wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari katika kiwanda cha kuongeza thamani ya mchele cha Salagulwa kilichopo katika halmashauri hiyo huku mkuu wa idara ya kilimo na uvuvi wa halmashauri hiyo Alphonce Bagamabyaki akisema serikali kwa kushirikiana na wadau imeendelea kuboresha sekta ya kilimo kwa kujenga kiwanda cha kuongeza thamani ya mchele.

Sauti ya afisa kilimo na mkuu wa idara ya kilimo Geita DC
Kiwanda cha kuongeza thamani ya mchele kilichopo Salagulwa wilayani Geita. Picha na Mrisho Sadick

Halmashauri ya wilaya ya Geita ina hekta zaidi ya elfu 23 za kuzalisha zao la mpunga huku baadhi ya wakulima wa mpunga katika eneo hilo Daniel Daud na John Mussa wakiiomba serikali kuharakisha uboreshaji wa miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji na upatikanaji wa pembejeo za kilimo ili kufikia malengo.

Sauti za wakulima

Ziara hiyo ya wahariri wa vyombo vya habari ni kuelekea katika maonesho ya kitaifa ya sita ya madini mkoani Geita ambayo yanatarajia kuanza Septemba 20 mwaka huu.