Storm FM

Bodaboda Geita wagoma kuzika wakiwadai rambirambi viongozi wao

29 September 2023, 10:30 pm

Waendesha bodaboda kutoka maegesho mbalimbali Geita. Picha na Zubeda Handrish

Suala la kupewa pesa pungufu unapotokea msiba wa bodaboda mwenzao katika chama cha bodaboda mkoa wa Geita, limewaibua bodaboda hao na kuamini viongozi wao wana kawaida ya kula rambirambi.

Na Zubeda Handrish- Geita

Waendesha boda boda mkoani Geita wamegoma kufanya mazishi ya boda boda mwenzao aliyefahamika kwa jina la Dotto Abeli mkazi wa Nyantorotoro mjini Geita, kwa kudai uongozi wao unakula pesa za rambirambi zinapochangishwa kutoka katika maegesho yao.

Wameyasema hayo leo katika ofisi kuu ya bodaboda hao iliopo mtaa wa Misheni mjini Geita wakiwasilisha mwili wa bodaboda mwenzao katika ofisi hiyo, wakidai kuna pesa zimepungua walizopwa kumaliza msibao huo hivyo viongozi hao wazitoe na wajitoe madalakani.

Baadhi ya wandesha bodaboda wakiwa kwenye gari lililobeba mwili wa mpendwa wao mbele ya ofisi yao ya mkoa. Picha na Zubeda Handrish

Juhudu za kuwapata viongozi wanaotuhumiwa zinaendelea, huku aliyekuwa Katibu wa umoja huo Fred Fideli Amezungumzia hali ilivyokuwa.

Sauti ya tukio zima la bodaboda hao lilivyotokea.

Mwenyekiti wa vijana Chama cha Mapinduzi CCM Manjale Magambo amefika katika ofisi hiyo ya bodaboda mkoa wa Geita na kutuliza ghasia hizo, huku akitoa kiasi cha sh laki tano kumaliza msiba wa mpendwa wao na kuaahidi kikao kikubwa siku ya Jumapili tarehe moja na kusikiliza kero zao.

Mwenyekiti wa vijana Chama cha Mapinduzi CCM Manjale Magambo, akizungumza na bodaboda mbele ya ofisi yao ya mkoa. Picha na Zubeda Handrish

Jeshi la pOlisi mkoa wa Geita, lilifika eneo la tukio na kuwataka bodaboda hao kuwa watulivu wakati suala lao linashughulikiwa.