Storm FM

Ushindani UMITASHUMTA Waongezeka Geita.

31 May 2021, 8:08 pm

Na Joel Maduka:

Afisa michezo Mkoa wa Geita, Carol Steven amesema kwa kiasi kikubwa ushindani kwa halmashauri sita zilizopo ndani ya Mkoa wa Geita ni mkubwa zaidi ukilinganisha na miaka ambayo wameshaendelea na michuano ya michezo ya UMITASHUMTA ambao umekuwa ukizikutanisha shule mbalimbali pamoja na halmashauri zilizopo ndani ya Mkoa huo. 

 Akizungumza na Storm Michezo kwenye viwanja vya shule ya wasichana ya Nyankumbu ambapo ndipo michezo hii iliendelea amesema  kila timu zinazocheza zimejipanga vizuri na kwamba mashindano na mchezo huo umekuwa na manufaa makubwa tangu kuanzishwa kwake kwani umeshatoa vijana ambao wanachezea timu mbali mbali na wengine wameendelea kuutangaza mkoa katika masuala ya michezo.