Storm FM

Vifusi barabarani kero kwa watumiaji wa vyombo vya moto Katoro

25 October 2023, 12:39 pm

Vifusi katika Barabara ya kuelekea soko kuu la Katoro. Picha na Daniel Magwina

Kuchelewa kurekebishwa kwa miundombinu ya barabara imekuwa kikwazo nakuzorotesha uchumi wa wa wananchi.

Na Kale Chongela:

Madereva pikipiki na Bajaji wanaotumia barabara ya  soko kuu la  mji mdogo wa  katoro wilayani Geita wamelalamikia uwepo wa vifusi katikati ya barabara hilo hali ambayo inakwamisha shughuli za usafirishaji.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti  baadhi ya madereva hao wamesema kutokana na changamoto ya vifusi hivyo inakwamisha utendaji wa kazi zao za kusafirisha abiria huku wakiiomba serikali ya wilaya ya Geita kuwasaidia kutatua changamoto hiyo. 

Sauti ya Madereva
Vifusi katika Barabara ya kuelekea soko kuu la Katoro. Picha na Daniel Magwina

Meneja wa wakala wa barabara za mjini na vijini TARURA Wilaya ya Geita  Mhandisi Bahati Subeya  amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo nakusema kuwa mkandarasi aliyekuwa akikarabati barabara hiyo alipata changamoto nakusimama kufanya kazi kwa muda nakwamba kuanzia wiki ijayo atakuwa kazini.

Sauti ya Meneja wa TARURA