Storm FM

Vyanzo vya maji asili siyo salama zaidi kipindi hiki cha mvua Geita

23 January 2024, 5:55 pm

Wajumbe wa kamati ya siasa wakifanya majaribio katika mradi wa maji katoro. Picha na Mrisho Shabani

Serikali wilayani Geita imeendelea kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji safi ili kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.

Na Mrisho Shabani:

Serikali wilayani Geita imewataka wakazi wa Kata za Katoro , Ludete na Nyamigota wilaya humo kuepuka kutumia maji ya kwenye vyanzo vya asili nabadala yake watumie mradi mkubwa wa maji ambao umeanza kutumika kwa majaribio ili kuepuka mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.

Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Geita Cornel Magembe wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Katoro mbele ya kamati ya siasa ya Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Geita iliyokuwa katika eneo hilo kufuatilia utekelezaji wa ilani ya CCM.

Mkuu wa wilaya ya Geita katikati akizungumza na wananchi wa katoro juu ya matumizi ya maji yakwenye mradi huo. Picha na Mrisho Shabani.
Sauti ya Mkuu wa wilaya

Kwa upande wake katibu mwenezi wa CCM Wilaya ya Geita ameiomba mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Geita GEUWASA kuhakikisha inaongeza kasi ya usambazi wa maji hayo kwa wananchi.

Sauti ya katibu Mwenezi wilaya ya Geita

Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kaimu Mkurugenzi wa GEUWASA Mhandisi Issack Mgeni amesema kwasasa upo katika hatua ya majaribio na umegharimu zaidi ya Bilioni 6 ambao utahudumia kata za Katoro, Ludete , Nyamigota wilayani Geita na Buseresere wilayani Chato.

Sauti ya kaimu mkurugenzi GEUWASA
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Geita akizungumza na wananchi wa katoro.Picha na Mrisho Shabani.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Geita Barnabas Mapande ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha za utekelezaji wa mradi huo  wa maji kutoka ziwa victoria huku akiwasisitiza wananchi kuepuka kutumia maji yasiyo salama.

Sauti ya Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Geita