Storm FM

Nyumba zaidi ya 100 zaezuliwa na upepo Nyang’hwale, mmoja afariki

18 October 2023, 10:53 am

Moja ya Nyumba iliyoharibiwa na Mvua iliyoambata na upepo mkali katika kijiji cha Lubando.Picha na Mrisho Sadick

Tangu kuanza kwa msimu wa mvua mwaka huu imeendelea kuleta madhara kwa baadhi ya wananchi Mkoani Geita huku chanzo cha madhara hayo ni uduni wa makazi.

Na Mrisho Sadick:

Mvua iliyoambatana na upepo mkali iliyodumu kwa dakika 30 imeezua na kuharibu nyumba zaidi ya 100 katika vijiji vinne vya kata ya Shabaka huku ikisababisha kifo cha mtu mmoja wilayani Nyang’hwale mkoani Geita.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Oktoba 16 mwaka huu na kusababisha uharibifu mkubwa wa nyumba za wakazi wa vijiji vya Nyamgogwa, Ihushi, Mhama, Shabaka huku katika kijiji cha Lubando mbali na kuharibu makazi ya watu imesababisha kifo cha Mathias Nkomola mwenye umri wa miaka zaidi ya 50  aliyeangukiwa na ukuta wa Nyumba wakati wa tukio.

Sauti ya wahanga wa tukio
Wananchi wakiwa msibani baada ya mpendwa wao kuangukiwa na ukuta wa nyumba wakati wa tukio katika kijiji cha Lubando.Picha na Mrisho Sadick

Diwani wa kata ya Shabaka Karimu Chasama ametembelea kaya za waathirika hao ikiwemo choo cha shule ya msingi Lubando na darasa moja katika shule ya msingi Mhama huku akiiomba serikali kuwasaidia wahanga wa tukio hilo.

Sauti ya Diwani na Mtendaji wa Kijiji Lubando
Moja ya Nyumba iliyoharibiwa vibaya na mvua iliyoambatana na upepo Mkali Kijiji cha Lubando.Picha na Mrisho Sadick