Storm FM

Walioanza mipango ya kuwaozesha watoto wa kike Nyang’hwale waonywa

17 September 2023, 2:20 pm

Wahitimu darasa la saba shule ya Msingi Roya Familiy wakiwa katika Mahafali. Picha na Mrisho Sadick

Wilaya ya Nyang’hwale imeanza kudhibiti changamoto ya watoto wa kike kuozeshwa baada ya kumaliza mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi mwaka huu.

Na Mrisho Sadick:

Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita Grace Kingalame ametoa onyo kwa wazazi na walezi walioanza mipango ya kuwaozesha watoto wao wa kike waliohitimu elimu ya msingi mwaka huu kuwa watachukuliwa hatua kali ikiwemo kufikishwa mahakamani.

Mhe Kingalame ametoa kauli hiyo katika mahafali ya saba ya shule ya msingi Royal Family iliyopo Geita mjini ambapo amesema kuna baadhi ya wazazi na walezi wameanza mipango ya kuwaozesha watoto wao wa kike waliohitimu elimu ya msingi  nakuwataka kuacha mipango hiyo mara moja.

Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale Grace Kingalame akizungumza na Storm FM. Picha na Mrisho Sadick
Sauti ya Mkuu wa wilaya

Shule ya msingi Royal Family imeanzishwa tangu 2016 , na mwaka huu  wanafunzi 67 wamehitimu Darasa la Saba huku Mkurugenzi wa Shule hiyo Mhandis Lazaro Philipo akisema wanafunzi katika Shule hiyo wanawajenga kujiajiri, kuwa na maadili pamoja na hofu ya Mungu.

Sauti ya Mkurugenzi Royal Family