Storm FM

Wananchi washiriki kutengeneza madawati Geita

15 April 2021, 6:00 pm

Na Paul Lyankando:

Serikali ya kijiji cha Ikunguigazi wilayani mbogwe mkoani Geita kwa kushirikiana na wananchi wameendelea kutengeneza madawati ili kuondoa changamoto ya wanafunzi zaidi 890 kusomea chini.

Mwenyekiti wa kijiji cha Ikunguigazi Bw Jumanne Manyasa amesema kwa kushirikiana na wananchi wameendelea kutengeneza n=madawati 100 kwa wanafunzi wa shule ya msingi ikunguigazi huku mpaka sasa wamekamilisha madawati 60 ili kuondoa changamoto ya madawati  kwa watoto.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wamesema wataendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali zinazoanzishwa na uongozi wa kijiji lakini wakaiomba serikali kuwashika mkono katika baadhi ya miradi wanayoanzisha wananchi.

Hata hivyo mwalimu mkuu katika shule hiyo mwalimu Christopher Mwita amewashukuru wananchi kwa kujitolea kutengeneza madawati ambapo amesema mara baada ya kukamilika kwa madawati hayo 100 upungufu itakuwa ni madawati 12.