Storm FM

Wananchi wapewa rai kufunika visima

5 July 2023, 8:28 am

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Geita Hamis Shabani Dawa. Picha na Kale Chongela

Matukio ya watoto na watu wazima pamoja na wanyama kutumbukia kisimani au kwenye mashimo yameonekana bado ni changamoto mkoani Geita, kiasi cha Jeshi la Polisi kuwakumbusha wananchi kufunika visima na mashimo hayo ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.

Na Kale Chongela -Geita

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Geita limewaagiza wamiliki wa visima na mashimo yaliyo wazi kuhakikisha wanayafunika kabla ya msimu wa mvua kuanza ili kuepuka matukio ya watu ikiwemo watoto kutumbukia.

Agizo hilo limetolewa na Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Geita Hamis Shabani Dawa kufuatia uwepo wa matukio ya watu na mifugo kutumbukia kwenye visima na mashimo yaliyo wazi na kufariki na kwamba Jeshi hilo halitawavumilia watu wote watakao kaidi agizo hilo.

Sauti ya Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Geita Hamis Shabani Dawa

Nao wananchi Mjini Geita wamekiri baadhi ya visima na mashimo kuwa wazi na kuahidi kuwa mabalozi wazuri wa hilo na kufunika visima katika Makazi ya yao.