Storm FM

Nyankumbu Girls yang’ara kuelekea kuanza kwa ligi kuu

10 August 2023, 1:03 pm

Uwanja wa Nyankumbu Girls, Geita. Picha na Zubeda Handrish

Kufuatia uharibu uliofanyika na watu wasiojulikana katika Dimba la Nyankumbu Girls, ukarabati mkubwa umefanyika kwaajili ya klabu ya Geita Gold FC kuutumia kwenye michezo ya ligi kuu ya NBC.

Na Zubeda Handrish- Geita

Kuelekea kuanza kwa msimu mpya wa 2023/24 wa ligi kuu ya NBC Agosti 15, 2023, ukarabati unaendelea katika Dimba linalotumiwa na Wachimba Dhahabu kutoka hapa mkoani Geita, Geita Gold FC kwaajili ya matumizi ya msimu mpya.

Jengo la Uwanja wa Nyankumbu Girls. Picha na Zubeda Handrish
Sauti ya mtangazaji wa Storm FM Zubeda Handrish na Msimamizi wa Uwanja wa Nyankumbu Girls Wilberty Zakaria Ngasa

Mkurugenzi Mtendaji wa Ngasa Field Engineering construction ambaye ni Msimamizi anaehusika kufanya ukarabati katika Dimba hilo, Wilberty Zakaria Ngasa anatolea ufafanuzi wa ukarabati huo.

Msimamizi wa Uwanja wa Nyankumbu Girls Wilberty Zakaria Ngasa. Picha na Zubeda Handrish

Geita Gold FC inaanzia ugenini michezo yake 3 ya mwanzo wa ligi ikifungua Dimba la michezo ya Ligi kuu ya NBC na Ihefu SC ya Jijini Mbeya, kisha kufuatia Kigoma kukipiga na Mashujaa FC na kumalizia Kagera dhidi ya Kagera Sugar na baada ya hapo watarejea katika Dimba la nyumbani, Nyankumbu Girls.