Storm FM

Kilometa 17 za lami kumaliza changamoto ya miundombinu ya barabara mjini Geita

26 October 2023, 4:18 pm

Meneja wa TARURA wilaya ya Geita Mhandisi Bahati Subeya akizungumza katika mkutano wa TACTIC. Picha na Kale Chongela

Baada ya wananchi wa baadhi ya maeneo ya Halmashauri ya Mji wa Geita kulia na changamoto ya miundombinu ya barabara sasa serikali imesikia kilio chao.

Na Kale Chongela:

Halmashauri ya mji wa Geita kupitia mradi wa uboreshaji miji TACTIC imeanza ujenzi wa barabara kilometa 17 kwa kiwango cha lami ili kuondoa changamoto ya usafirishaji watu na bidhaa ndani ya mji wa Geita.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa  Wakala wa barabara za mjini na vijini TARURA wilaya ya Geita Mhandisi  Bahati Subeya katika mkutano uliowakutanisha viongozi mbalimbali wa kata nne ambazo zitanufaika na mradi huo.

Sauti ya Meneja TARURA
Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Geita Mhandisi Constantine Morandi akizungumza katika mkutano wa TACTIC. Picha na Kale Chongela

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita Costantine Morandi ametumia fursa hiyo kuwataka wakandarasi kuanza kutelekeza barabara hizo  kwa wakati  kwani yapo baadhi ya maeneo korafi hivyo inatakiwa  kazi ifanyika kwa kasi

Sauti ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Geita

Mkuu wa wilaya ya Geita Mhe. Cornel Magembe ametoa msistizo kwa TARURA Kujenga desturi ya kukagua barabara hizo kila wakati ili zijengwe kwa kiwanga kinachotakiwa.

Mkuu wa wilaya ya Geita Cornel Magembe akizungumza katika mkutano wa TACTIC. Picha na Kale Chongela
Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Geita

Barabara hizo ni Mkolani – Mwatulole Kilometa 5.9 , Nyankumbu – Kivukoni Kilometa 3.9 , Nguzombili -Samandito – Emma – Mama Kengele kilometa 3.3 na Mwatulole – Nshinde – Twiga – GGR 3.9.