Storm FM

Kilio cha kupanda bei ya mafuta chawafikia abiria

9 August 2023, 1:03 pm

Waendesha vyombo vya usafirishaji Joshoni, Geita. Picha na Zubeda Handrish

Mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Agosti 2023 yamechagiza waendesha vyombo vya moto mjini Geita kuongeza bei kiholela.

Na Zubeda Handish- Geita

Baadhi ya wananchi mkoani Geita wamezungumzia juu ya kadhia wanayokumbana nayo kwa waendesha vyombo vya usafiri ya kupandishiwa bei kinyume na utaratibu.

Hayo yanajiri baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), kutangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini, zilizoanza kutumika tangu Jumatano ya Agosti 2, 2023 saa 6:01 usiku.

Sauti ya wananchi/wateja mjini Geita

Kufuatia malalamiko hayo, waendesha vyombo vya moto hususani bajaji wanaopatikana katika egesho la Joshoni Nyakumbu mjini Geita, wamefunguka wakidai kupanda kwa bei ya mafuta ni chanzo.

Sauti ya waendesha vyombo vya usafirishaji Joshoni, Geita
Waendesha vyombo vya usafirishaji Joshoni, Geita. Picha na Zubeda Handrish

Kwa upande wake Afisa Tawala Msaidizi Huduma kwa Wateja EWURA CCC mkoa wa Geita, Wadi Omary amekiri kuongezeka kwa bei ya mafuta, huku akiwasihi wenye vituo vya mafuta kufuata utaratibu wa bei hizo.

Sauti ya Afisa Tawala Msaidizi Huduma kwa Wateja EWURA CCC

Katika hatua nyingine ametolea ufafanuzi pia kwa vyombo vya usafiri vinavyopandisha bei kiholela.

Sauti ya Afisa Tawala Msaidizi Huduma kwa Wateja EWURA CCC

Mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Agosti 2023 yameonesha kupanda kwa bei kunatokana na changamoto za upatikanaji wa Dola za Marekani, mabadiliko ya sera za kikodi, kushuka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola ya Marekani, ongezeko la gharama za mafuta katika soko la dunia na gharama za uagizaji wa mafuta.