Storm FM

GGML yatimiza ahadi ya basi jipya kwa klabu ya Geita Gold FC

14 October 2023, 12:05 pm

Basi jipya la Geita Gold FC aina ya Youtong F 12. Picha na Zubeda Handrish

Changamoto ya usafiri baada ya klabu ya Geita Gold FC kupanda Ligi kuu ya NBC msimu wa 2021/22, umepelekea mdhamini mkuu wa klabu hiyo GGML kuahidi basi litakalowarahisishia kusafiri.

Na Zubeda Handrish- Geita

Mgodi wa dhahabu wa Geita Gold Mine Limited (GGML) ambao pia ni mdhamini mkuu wa klabu ya Geita Gold FC inayoshiriki Ligi kuu ya NBC ya hapa mkoani Geita, umeikabidhi klabu hiyo basi jipya aina ya Youtong F 12 lenye thamani ya sh. milioni 500 ili kuirahisishia klabu katika safari zake, ambapo ilikuwa ahadi kwa klabu hiyo tangu msimu wa kwanza ilipofanikiwa kupanda Ligi kuu.

Mwenyekiti wa klabu ya Geita Gold FC Leonard Shiganga Bugomola kushoto na Mkurugenzi Mtendaji wa GGML Terry Strong wakikabidhiana hati za umiliki wa basi jpya. Picha na Zubeda Handrish

Mgeni rasmi katika hafla hiyo ya makabidhiano Waziri wa Madini Antony Mavunde ametoa pongezi kwa mgodi wa GGML huku akiendelea kuwasisitiza kudumisha ushirikiano kupitia CSR na wanageita.

Sauti ya Waziri wa Madini Antony Mavunde

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Terry Strong amefurahia kuungana na klabu hiyo na wanageita katika tukio hilo la kihistoria la kuikabidhi Geita Gold FC basi walilowaahidi.

Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji wa Terry Strong

Mwenyekiti wa klabu hiyo Leonard Shiganga Bugomola kwa niaba ya uongozi wa klabu na wachezaji ameushukuru mgodi wa GGML kwa tukio hilo kubwa kwa soka la mkoa wa Geita na klabu hiyo huku akiahidi makubwa na kuendeleza ushirikiano.

Sauti ya Mwenyekiti wa klabu ya Geita Gold FC Leonard Shiganga Bugomola