Storm FM

Msako waganga wanaosababisha mauaji Geita

9 April 2024, 6:01 pm

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita SACP Safia Jongo akizungumza na wakazi wa Iparamasa Chato. Picha na Mrisho Sadick

Matukio ya watu kudaiwa kukamatwa hovyo na wananchi katika kijiji cha Iparamasa Chato yamemuibua Kamanda wa Jeshi la Polisi.

Na Mrisho Sadick – Geita

Jeshi la polisi Mkoani Geita linaendelea  kuwasaka nakuwakamata waganga wa tiba asili ambao wanafanya ramli chonganishi katika maeneo mbalimbali mkoani humo ambazo zimekuwa zikileta madhara katika jamii ikiwemo mauaji.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Geita kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Safia Jongo ametoa kauli hiyo katika kijiji cha Iparamasa wilayani Chato kufuatia malalamiko ya baadhi ya wakazi wa eneo hilo ya uwepo wa vitendo vya kamata kamata.

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano wa Mkuu wa Mkoa Iparamasa Chato. Picha na Mrisho Sadick
Sauti ya Kamanda wa Polisi Geita

Awali wakitoa malalamiko mbele ya mkuu wa mkoa wa Geita baadhi ya wakazi wa Kata ya Iparamasa wametaka kufahamu juu ya vitendo vya watu kukamatwa nakupelekwa vituo vya polisi ambavyo viko nje na wilaya hiyo.

Sauti ya wananchi Chato

Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela amewataka wakazi wa eneo hilo kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la Polisi kwa kuwafichua waganga wanaoendelea kufanya ramli chonganishi.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Geita
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mrtine Shigela akizungumza na wakazi wa Iparamasa Chato . Picha na Mrisho Sadick