Storm FM

Joyce auawa kisha sehemu zake za siri kunyofolewa Mbogwe

26 October 2023, 3:50 pm

Kaburi la Joyce aliyeuawa kikatili katika kijiji cha Ikobe wilayani Mbogwe Mkoani Geita. Picha na Nicholaus Lyankando

Ramli chonganishi zimeendelea kusababisha mauaji maeneo mbalimbali hapa nchini huku serikali ikitakiwa kupambana na suala hilo kuokoa maisha ya watu hususani maeneo ya vijijini.

Na Mrisho Sadick:

Mwanamke Joyce Luhedeka mwenye umri wa miaka (51)  Mkazi wa kijiji cha Ikobe wilayani Mbogwe Mkoani Geita ameuawa kikatili kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni kisha kuondolewa sehemu zake za siri.

Tukio hilo la kikatili  limetokea majira ya usiku wakati mwanamke huyo akitoka katika shughuli zake za kuuza ndizi ,mwili wake umekutwa umetelekezwa kando ya mashamba ya mpunga mkabala na nyumbani kwakwe huku baadhi ya mashuhuda wa tukuio hilo wakisema.

Sauti ya shuhuda na jirani

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho amekiri kutokea kwa tukio hilo huku Mtoto wa mama huyo akieleza namna alivyopata taarifa.

Sauti ya Mwenyekiti na Mtoto wa marehemu

Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Geita kamishna msaidizi wa Polisi ACP Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio nakwamba wanamshikilia Dada wa marehemu na mganga wa kienyeji ambae ndie aliwaagiza sehemu za siri za mwanamke huyo wakimtuhumu marehemu kuhusika na kifo cha binti yao.

Sauti ya Kamanda wa Polisi Geita RPC
Picha ya kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Geita ACP Safia Jongo. Picha na Evance Mlyakado