Storm FM

Anusurika kipigo baada ya kukutwa kwenye makazi ya watu bila ya nguo.

4 January 2023, 8:19 am

Na Mrisho Sadick:

Mwanamke mmoja ambae hakufahamika jina lake Mkazi wa Mtaa wa Nyerere Road mjini Geita amenusurika kipigo kutoka kwa wananchi wa mtaa wa Uwanja Kata ya Nyankumbu baada ya kukutwa nje ya makazi ya mtu akiwa mtupu akahisiwa kuwa ni mchawi.

Baadhi ya Mashuhuda wa tukio hilo wamesema baada ya kumkuta Mwanamke huyo akiwa katika hali hiyo isiyo ya kawaida walijaribu kumhoji na alikuwa akisema ameachwa na wenzake ambao alikuwa nao kwenye ungo na anasubiri wamfuate.

Katibu wa Balozi wa Shina hilo Shija Limbu amewaasa wananchi wa mtaa huo kutojichukulia hatua mkononi kwa kuadhibu watu pasipokufuata utaratibu kwani inaonekana Mwanamke huyo alikuwa na matatizo ya akili.