Storm FM

Vijana waaswa kuacha matumizi ya madawa ya kulevya ili kuepuka utegemezi kwa familia

8 September 2023, 1:43 pm

Picha na TMKU- Tanzania

Utegemezi kwa familia imetajwa kuwa moja ya sababu inayosababishwa na matumizi ya madawa ya kulevya kwa vijana.

Na Daniel Magwina- Geita

Kufuatia wimbi la vijana kuingia katika matumizi ya madawa ya kulevya baadhi ya wananchi mkoani Geita mapema leo hii, wamesema kuwa madawa ya kulevya yanasababisha kupoteza nguvu kazi kwa taifa, kuwa tegemezi, pamoja na kupata madhara mbalimbali ya kiafya.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema kuwa vijana ambao wanajihusisha na madawa ya kulevya hawana budi kuacha tabia hiyo.

Sauti ya wananchi wa Geita wakizungumzia athari za madawa ya kulevya kwa jamii

Wananchi hao pia wameviomba vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha wanadhibiti kikamilifu wauzaji na wasambazaji wa madawa hayo.

Kwa upande wake Mganga Mfawithi wa halmashauri ya mji wa Geita, amesema kuwa madawa ya kulevya yana madhara mbalimbali kwa mtu ambae anatumia.

Sauti ya Mganga Mfawithi wa halmashauri ya mji wa Geita

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na Madawa na Uhalifu,  UNODC mwaka 2019 ilitoa ripoti iliyoonesha idadi ya watu wanaotumia mihadarati duniani imeongezeka, na kwamba mwaka 2020 pekee duniani kote watu milioni 275 walitumia mihadarati ikiwa ni ongezeko la asilimia 22.