Storm FM

Bei ya nafaka yapanda Geita

25 August 2023, 9:08 am

Hali ya nafaka soko la Nyankumbu, Geita. Picha na Adelina Ukugani

Kupanda kwa bei ya nafaka imechangia kupungua kwa kasi ya biashara katika soko la Nyankumbu mjini Geita.
Na Adelina Ukugani- Geita

Wafanyabiashara wa nafaka katika soko la asubuhi la Nyankumbu mjini Geita wamelalamikia kupanda kwa bei ya mazao hayo hali inayochangia biashara zao kudorora kutokana na wateja kushindwa kuhimili bei.

Wafanyabiashara wa nafaka soko la Nyankumbu, Geita

Baadhi ya wafanyabiashara hao wameiambia Storm FM kuwa biashara hiyo imekuwa ngumu kutokana na mazao ya nafaka kuongezeka bei kutoka kwa wakulima.

Bei ya nafaka katika soko la Nyankumbu Geita. Picha na Adelina Ukugani

Mwenyekiti wa soko hilo Mchele Mhangwa amesema nafaka zimepanda bei kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta nakwamba inawalazimu kupandisha bei kutokana na gharama za usafirishaji wa bidhaa kuwa juu.

Bei ya nafaka kwa siku ya jana upande wa Maharage kilo moja iliuzwa kwa shilingi 2,500, Mahindi kilo moja ni shilingi 1,000, mchele 2,200 karanga 3,000, bei hizi hubadilika kulingana na upatikanaji wa mazao hayo nakupanda kwa gharaza za usafirishaji.