Storm FM

Bilioni 1.4 kujenga kiwanda cha kuzalisha vifaranga vya samaki Chato

28 November 2023, 1:18 pm

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe, Abdallah Ulega akifungua rasmi tamasha la Chato Utalii Festival kwaniaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii. Picha na Mrisho Sadick

Kutokana na ukuaji wa uzalishai wa zao la samaki, serikali imetenga bajeti kwaajili ya ujenzi wa kiwanda.

Na Mrisho Sadick- Geita

Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imetenga kiasi cha zaidi ya Bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kuzalisha vifaranga vya samaki wilayani Chato Mkoani Geita, ili kufungua fursa kwa wananchi za ufugaji wa samakiĀ  wa kutumia vizimba ndani ya ziwa Victoria.

Sauti ya Mwanahabari wa Storm FM Mrisho Sadick, akielezea ufunguzi wa tamasha la Chato Utalii Festival

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe, Abdallah Ulega ametoa kauli hiyo wakati akifungua rasmi tamasha la Chato Utalii Festival kwaniaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii katika viwanja vya Magufuli Chato mjini ambalo limeanza Novemba 26 hadi Disemba 3 mwaka huu na linaongozwa na kaulimbiu isemayo Utalii ni Uchumi.

Wananchi Chato wakiwa katika ufunguzi wa tamasha la Chato Utalii Festival wilayani Chato. Picha na Mrisho Sadick

Mkuu wa wilaya ya Chato Deusdedit Katwale amesema lengo la kuanzisha tamasha hilo ni Kukuza Utalii nakufungua fursa za uwekezaji katika wilaya hiyo nakwamba mataifa ya nje yanayoshiriki ni pamoja na Kenya , Uganda , Rwanda na Burundi huku mdhamini mkuu wa tamasha hilo akiwa ni Benki ya NMB.