Storm FM

RC Geita azindua Chanjo kwa kuchanjwa.

4 August 2021, 7:49 pm

Na Mrisho Sadick:

Mkuu wa Mkoa wa Geita Bi Rosemary Senyamule ametoa onyo kwa watumishi wa afya na vituo binafsi vyakutolea huduma za Afya watakaobainika wakiwauzia wananchi chanjo ya kujikinga na corona.

Mkuu wa Mkoa huyo  Senyamule ametoa kauli hiyo  wakati akizindua zoezi la utoaji wa chanjo ya kujikinga na gonjwa wa Corona Mkoani Geita kwa Makundi lengwa wakiwemo Wazee, watumishi wa Afya na watu wenye magonjwa sugu ambapo amesema Mkoa wa Geita umepokea dozi elfu hamsini za chanjo kwa hatua ya kwanza.