Mwenge wa uhuru kukagua miradi ya Tsh. bilioni 32.2 Geita
30 September 2024, 5:59 pm
Mwenge wa uhuru umepokelewa katika mkoa wa Geita na kuanza mbio zake wilayani Chato kwa shughuli ya kukagua, kuzindua, kutembelea na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Na: Kale Chongela – Geita
Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela leo Septemba 30, 2024 amekabidhiwa mwenge wa Uhuru na mkuu wa mkoa Kagera Fatma Mwasa katika kijijiji cha Katete kata ya Bwongera wilaya ya Chato mkoani Geita.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa mwenge wa uhuru RC Shigela amesema mwenge wa uhuru utatembea kilomita 826.6 ndani ya mkoa wa Geita.
Ukiwa mkoani Geita pia utaweka jiwe la msingi katika jiwe la msingi katika miradi 18, kuzindua miradi 22, kutembelea na kuona miradi 25 yenye thamani ya shilingi Bilioni 32.2.