Storm FM

Wajasiriamali zaidi ya 100 wapata hasara.

4 May 2023, 8:42 am

Na Kale Chongela:

Zaidi ya Wajasiriamali 100 waliopo njia panda mamlaka ya mji mdogo wa Katoro wilaya ya Geita  na mkoani Geita wameacha biashara hiyo kutokana na mzunguko kuwa mdogo.

Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa umoja wa wajasiriamali waliopo katika eneo hilo  Bw. Eliasi Buhumbi ambapo amesema baada ya kufanya tathimini imebainika kuwa miongoni mwa wajasriamali zaidi ya 300 kati ya hao 100 wameacha kufanya biashara hiyo.

Aidha Bw. Buhumbi amesema kupitia vikao vyao wamekuwa wakielimishana wao kwa wao ili kuendelea kuondokana na changamoto hiyo.