Storm FM

Wataalam MSD watembelea Hospitali ya Kanda Chato

13 July 2023, 1:25 pm

Wataalam wa MSD wakiwa katika picha ya pamoja. Picha na Hospitali ya Rufaa ya kanda Chato.

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato imeendelea kuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wanaozunguka wilaya hiyo huku changamoto mbalimbali zinazoikabili ikiwemo dawa na vifaa tiba zikiendelea kupatiwa ufumbuzi kwa haraka.

Na Mrisho Sadick

Wataalam kutoka Bohari ya Dawa (MSD) wamefika katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato na kukutana na Menejimenti ya Hospitali hiyo kwa lengo la kujadili maendeleo na changamoto ambazo Hospitali  hiyo inakutana nazo kutoka MSD.

Moja ya changamoto zilizojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na upatikanaji wa Dawa, vifaa tiba na vitendanishi ili zifanyiwe kazi na kutatuliwa ili kuongeza ufanisi katika utendaji wa kuwahudumia wananchi.

Wataalamu wa MSD wakiwa wakiwa Hosptali ya Kanda Chato. Picha na Hospitali ya Rufaa ya kanda Chato.

Akizungumza katika kikao hicho meneja rasilimali watu kutoka MSD amesema kikao hicho kinalenga kuboresha huduma katika Hospitali hiyo kwa kujua changamoto zilizopo ili zitatuliwe haraka ili waanchi wanaofika katika eneo hilo wasikose huduma.

Sambamba na hilo ameiomba Hospitali hiyo kufanya maoteo sahihi ya bidhaa za Afya ili kuipa MSD auheni katika utoaji huduma kwa haraka zaidi ,wakati sahihi na weledi na kwendana na uhitaji wa wananchi wanaohudumiwa.