Storm FM

Shigela: Viongozi wa dini wana mchango mkubwa katika amani ya nchi

14 July 2023, 1:28 pm

Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa Injili CCM Kalangalala Geita mjini. Picha na Kale Chongela

Inaelezwa kuwa utulivu , amani , umoja na mshikamano katika taifa umechangiwa kwa kiasi kikubwa na viongozi wa dini kuendelea kuwajenga kiimani wananchi.

Na Kale Chongela:

Serikali mkoani Geita imesema inatambua mchango wa viongozi wa dini katika kuleta umoja na amani nchini nakuahidi kuendelea kuwaunga mkono katika shughuli zao zakufikisha neno la mungu kwa wananchi.

kauli imetolewa na mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela katika uzinduzi wa mkutano wa Injili wa kanisa la  Efatha,  katika uwanja wa CCM Kalangalala mjini Geita.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela akiwa kwenye Mkutano wa Injili CCM Kalangalala Geita mjini. Picha na Kale Chongela
Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita kamishna msaidizi wa Polisi ACP Safia Jongo amesema uwepo wa mikutano ya Injili  utasaidia watu  kuendelea kujifunza mafundisho mema nakuacha matendo mauvu.

Sauti ya Kamanda wa Polisi Geita ACP Safia Jongo

Kwa upande wake  Mtume Nabii Josephat Mwingila amesema injili ndo msingi Mkubwa wa mafanikio nakwamba ni vyema kila mmoja amjue mungu kuwa ndye mwokozi wa maisha yeke.

Mtume Nabii Josephat Mwingila akiwa kwenye Mkutano wa Injili CCM Kalangalala Geita mjini. Picha na Kale Chongela
Sauti ya Nabii Josephat Mwingila