Storm FM
Storm FM
13 August 2026, 1:58 pm

Serikali imeendelea kuboresha kituo cha Afya Iparamasa kwa kukarabati miundombinu mbalimbali ili kusaidia utoaji wa huduma za afya kwa wananachi.
Na: Ester Mabula
Kituo cha Afya Iparamasa kilichopo wilaya ya Chato mkoani Geita kimekabidhiwa gari la wagonjwa (Ambulance) lenye zaidi ya shilingi milioni 300 lililotolewa na serikali ili kuweza kusaidia wagonjwa wa dharura katika eneo hilo.
Hafla ya kukabidhi gari hilo imefanyika Agosti 12, 2026 katika kituo hicho, akitoa taarifa mbele ya mgeni rasmi Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Chato Ndg. Mandia Kihio amesema mradi huo wa kituo cha Afya umegarimu jumla ya shilingi milioni 741 zilizotengwa na kutolewa na serikali ikiwemo Milioni 105 zilizotumika kwaajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba na Milioni 45 kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya maji kupitia mradi wa Wash.

Mgeni rasmi, Mbunge wa Jimbo la Chato Kusini Mhe. Paschal Lucas Lutandula amesema ataendelea kuwa karibu na wananchi wake na kutimiza ahadi za kutatua changamoto alizotoa wakati wa kampeni huku akiahidi kujenga jengo la watumishi wa kituo hicho.
Baadhi ya wananchi wameipongzea na kuishukuru serikali sambamba na mbunge wa jimbo hilo kwa kuweza kuwasaidia kwa kuwapatia gari la wagonjwa kwani hapo awali walikuwa wakiteseka na kutumia gharama kubwa kwenda katika maeneo mengine iwapo itatokea dharura kwa wagonjwa.
