Storm FM

Kichanga chaokotwa kikiwa hai mtaa wa 14 Kambarage

13 August 2026, 5:02 pm

Mwananchi msamaria mwema aliyeokota mtoto huyo katika mtaa wa 14 Kambarage akiwa amembeba. Picha na Kale Chongela

Licha ya Jitihada za serikali kwa kushiriana na wadau na mashirika mbalimbali kupinga vitendo vya ukatili, bado baadhi ya watu wameendelea kufanya vitendo vya ukatili.

Na: Kale Chongela

Mtoto mchanga ameokotwa akiwa hai ambapo imedhaniwa kuwa ametupwa muda mfupi baada ya kuzaliwa katika mtaa wa 14 Kambarage, kata ya Buhalahala, halmshauri ya manispaa ya Geita mkoani Geita.

Tukio hilo limetokea Agosti 12, 2026 katika ubalozi wa shina namba 7 katika mtaa wa 14 kambarage ambapo baadhi ya wakazi wa eneo hilo waliokuwa karibu na eneo la tukio walifanikiwa kumuona mtoto huyo na kutoa taarifa hatua iliyowezesha mtoto huyo kuokolewa akiwa katika hali ya uhai.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa 14 Kambarage Bw. James Sanyenge amekiri kutokea kwa tukio hilo katika mtaa wake na kusema kuwa baada ya kujiridhisha walifanikiwa kumfikisha mtoto huyo katika hospitali ya manispaa ya Geita kwa matibabu zaidi.

Kaimu mganga Mfawidhi katika Hospitali ya manispaa ya Geita Bw. Kassim Msuya amekiri kumpokea mtoto huyo na kueleza kuwa baada ya kupokelewa amefanyiwa matibabu sambamba na vipimo na kwamba yupo kwenye uangalizi wa madaktari na anaendelea vizuri .

Sauti ya Kale Chongela na taarifa zaidi.