Storm FM
Storm FM
13 July 2026, 12:36 pm

Picha ya pamoja ya Jeshi la polisi kitengo cha Usalama barabarani, wafanyakazi wa Blue Coast na bodaboda. Picha na Kale Chongela
Kampeni hiyo ni sehemu ya jitihada za kampuni ya Blue Coast kwa kushirikiana Jeshi la Polisi kitengo cha usalama katika kujenga utamaduni wa usalama barabarani na kupunguza idadi ya ajali Mkoani Geita.
Na: Kale Chongela
Kampuni ya usafirishaji ya Blue Coast iliyopo Mkoani Geita kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani imeanzisha kampeni maalumu ya kuhamasisha usalama barabarani kwa lengo la kupunguza ajali na madhara yanayotokana na ajali hizo.
Akizungumza na Storm Fm Meneja wa kampuni ya Blue Coast Jeremia Musa amesema Kampeni hiyo inalenga kutoa elimu kwa madereva abiria pamoja na watumiaji wengine wa barabara kuhusu umuhimu wa kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwemo kufuata alama za barabarani, kuepuka mwendo kasi, kutoendesha gari wakiwa wamelewa.
Sauti ya Meneja wa kampuni ya Blue Coast
Akitoa Elimu ya usalama barabarani akiwa katika kata ya Nyankumbu manispaa ya Geita Sargent Lucas Rwechungula kutoka Jeshi la Polisi Kitengo cha usalama barabara Mkoani Geita amesema kuwa ajali nyingi zinaweza kuzuilika endapo kila mtumiaji wa barabara atazingatia wajibu wake.
Sauti ya Sargent Lucas Rwechungula kutoka Jeshi la Polisi Kitengo cha usalama barabarani
Hata hivyo Naibu katibu Mkuu wa umoja wa madereva bodaboda Mkoa wa Geita Bw George manyogote amesema kampeni hii inaenda kupunguza ajali barabarani .
Sauti ya Naibu katibu Mkuu wa umoja wa madereva bodaboda

Madereva bodaboda walioshiriki kampeni hiyo. Picha na Kale Chongela
Mkaguzi wa Jeshi la Polisi ambaye ni polisi kata wa kata ya Nyankumbu Farida Mandela amewataka madereva kuwa na nidhamu barabarani na kuweka mbele usalama wa maisha ya abiria na watumiaji wengine huku akiwataka kuendelea kulinda amani .
Sauti ya Mkaguzi wa Jeshi la Polisi ambaye ni polisi kata wa kata ya Nyankumbu