Storm FM

Msichana adaiwa mchawi baada ya kukutwa uchi nyakati za usiku

1 May 2021, 12:01 pm

Na Mrisho Sadick:

Mtoto anaekadiriwa kuwa na zaidi ya umri wa miaka 15 katika mtaa wa 14 Kambarage mjini Geita amewekwa chini ya ulinzi na wananchi baada ya kukutwa akiwa hana nguo nyakati za usiku kwenye makazi ya watu nakudaiwa kuwa alikuwa akifanya ushirikina yeye pamoja na shangangazi yake.

Akizungumza na Storm FM Mtoto huyo alionekana kama ni mtu ambae amechanganyiwa kutokana na mazungumzo yake kutokuwa yanaeleweka vizuri, huku akiwa hajulikani ametoka wapi hadi pale jeshi la polisi kwa kushirikiana na Ofisi ya serikali ya mtaa huo walipofika nakumchukua kisha kuondoka nae.

Msichana anaedaiwa Mchawi

Baadhi ya wakazi wa Mtaa huo akiwemo mchungaji wa kanisa la EAGT wamesema walimuona mtoto huyo majira ya saa 11 alfajiri akiwa uchi wa mnyama walipo jaribu kumhoji kuhusu hali hiyo alisema shangazi yake amemuacha nawalifika hapo kwa usafiri wa fisi.

Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa 14 kambarage mjini Geita Bw Maurid Mrisho amekiri kuwepo kwa tukio hilo nakutumia fursa hiyo kuishauri jamii kuachana na vitendo hivyo kwani ni hatari kwa usalama wa maisha yao.