Storm FM

Bilioni moja kumaliza adha ya maji Nyarugusu

17 May 2024, 9:53 am

Wakazi wa Kata ya Nyarugusu wakiwa kwenye mkutano wa MNEC. Picha na Mrisho Sadick

Changamoto ya upatikanaji wa maji safi bado ni changamoto kwa wananchi hususani wanaoishi vijijini huku serikali ikiendelea kukabiliana na changamoto hiyo.

Na Mrisho Sadick – Geita

Wakazi wa Kata ya Nyarugusu wilayani Geita wanatarajia kuondokana na changamoto ya kuchangia maji na wanyama katika mabwawa baada ya serikali kutoa fedha kiasi cha zaidi ya bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa mradi mkubwa wa maji katika Kata hiyo.

Wakizungumzia hatua hiyo kwenye mkutano wa Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa wa kupokea taarifa ya utekelezaji shughuli za maendeleo baadhi ya wakazi wa kata hiyo wameipongeza serikali kwa kuanza utekelezaji wa mradi huo ambao utaondoa changamoto nyingi ikiwemo ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo.

Sauti ya wananchi
Wakazi wa Kata ya Nyarugusu wakiwa kwenye mkutano wa MNEC. Picha na Mrisho Sadick

Afisa mtendaji wa Kata hiyo Lusekelo Mwaikenda amesema  mradi huo  umefikia asilimia 40 na utakuwa na tenki lenye lita za ujazo laki tatu.

Sauti ya afisa Mtendaji
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Evaristi Gervas akizungumza na wakazi wa Nyarugusu. Picha na Mrisho Sadick

kwa upande wake mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa Evarist Gervas amewataka wakazi wa kata hiyo kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya muungano wa tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwakuwa anasikiliza nakutatua kero zao kwa wakati.

Sauti ya MNEC