Storm FM

Maduka matatu yateketea kwa moto Bukombe

29 July 2023, 10:20 pm

Wananchi wakiwa harakati za kupambana kuzima moto . Picha na Alex Masele

Uduni wa vifaa vya uokozi kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Geita inachangia kulifanya Jeshi hilo kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi.

Na Alex Masele:

Maduka matatu ya wafanyabiashara katika mji wa Ushirombo Halmashauri ya wilaya Bukombe Mkoani Geita yameteketea kwa moto majira ya saa mbili usiku julai 29,2023 huku chanzo cha moto huo kikidaiwa kuwa ni umeme.

Baadhi ya wananchi walioshudia tukio hilo wameiomba serikali kuimarisha huduma ya Jeshi la Zimamoto na uokoaji wilayani humo ili kukabiliana na majanga ya mato kwakuwa kwasasa hawaoni msaada wa jeshi hilo.

Sauti za wananchi kwenye tukio

Diwani wa kata ya katente lilipotokea tukio hilo amewataka wakazi wa kata hiyo kuendelea kushirikiana inapotokea changamoto kama hiyo kwa kufuata maelekezo ya jeshi la zimamoto na uokoaji.

Sauti ya Diwani