Storm FM

Viongozi wa mamlaka ya mji wa katoro wilayani Geita wamuenzi JPM

2 April 2021, 3:45 pm

Baadhi ya viongozi wa mamlaka ya mji mdogo wa Katoro wilayani na Mkoani Geita  wamesema katika kumuenzi Hayati  Dkt John Pombe Magufuli watahakikisha wanafanya kazi kwa uadilifu.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa mtendaji wa kata ya Katoro wilayani Geita Bw Selemani Mahushi na kubainisha kuwa hayati Dkt Magufuli alisisitiza kuchapa kazi kwa bidii hivyo watanzania wanapaswa kumuenzi kwa kuendelea kufanya kazi kwa manufaa yao, jamii na taifa kwa ujumla.

Sanjari na hayo Bw  Mahushi ametumia fursa hiyo kuwataka wananachi wa eneo hilo kumuombea   Rais wa  awamu ya 6 wa Jamhuri  ya muungano wa Tanzania  Mhe, Samia Suluhu Hasani  kwa kazi ya kuwatumikia wa Tanzania .