Storm FM

Mwanamke aliyejeruhiwa na mume wake anaendelea vizuri

25 November 2023, 11:26 am

Mwanamke Justina Paul akiwa Hosptali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita. Picha na Kale Chongela

Bwana Colini mtendaji wa mtaa wa 14 kambarage ndiye aliyetolea taarifa tukio hilo la ugomvi wa mke na mume baada ya kutokea mtaani hapo.

Na Kale Chongela- Geita

Mwanamke Justina Paul ambaye alijeruhiwa kwa panga sehemu mbalimbali za mwili wake na mume wake katika Mtaa wa 14 kambarage kasha mume wake kujinyonga hadi kufa kisa wivu wa mapenzi anaendelea kupatiwa matibabu katika Hosptali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita.

Mganga Mfawidhi wa Hosptali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita Dkt Salum Mfaume amekiri kumpokea mwanamke huyo nakwamba kwa sasa anaendelea kupatiwa matibabu.

Sauti ya Mganga Mfawidhi wa Hosptali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita Dkt Salum Mfaume

Kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita ACP Adamu Maro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo kuku akitaja chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi.