Storm FM

Wazee nchini walaani vijana kuwalazimisha kuwarithisha mali

6 October 2023, 10:27 am

Wazee kutoka Mikoa mbalimbali hapa nchini wakiwa kwenye kongamano la wazee Mkoani Geita. Picha na Mrisho Sadick

Wazee Nchini wameiomba serikali kuingilia kati vitendo vya baadhi ya vijana wao kuwalazimisha kuwarithisha mali ili hali wako hai sababu ambayo inachangia wengi wao kufanyiwa vitendo vya ukatili ikiwemo mauaji pindi wanapokataa kufanya hivyo.

Suala la vijana kuwalazimisha wazee kuwarithisha mali ili hali wako hai limeendelea kuwakera wazee wengi hapa nchini huku wazee hao wakiiomba serikali kuingilia kati.

Na Mrisho Sadick:

Wakizungumza katika kongamano la kuelekea maadhimisho ya kitaifa ya siku ya wazee duniani Mkoani Geita, baadhi ya wazee hao wamesema wanaendelea kufanya tathimini juu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili wazee hapa nchini ikiwemo vitendo vya ukatili wa mali.

Sauti ya Wazee

Mwenyekiti wa Baraza la wazee Taifa Lameck Sendo amesema ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili wazee ikiwemo vitendo vya ukatili ameishauri serikali kuwashirikisha wazee kwenye vyombo vya maamuzi.

Mwenyekiti wa baraza la wazee taifa akiwa kwenye kongamano la wazee Mkoani Geita . Picha na Mrisho Sadick
Sauti ya Mwenyekiti Baraza la Wazee Taifa
Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela akiwa kwenye kongamano la Wazee . Picha na Mrisho Sadick

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela amewatoa hofu wazee hao huku akisema serikali ya awamu ya sita itaendelea kuwalinda nakuwathamini wazee wote hapa nchini.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa